Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu

Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Ayub Al-Answari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Ni haramu kwa mtu kumhama ndugu yake zaidi ya siku tatu, wanakutana, huyu akampuuza huyu na huyu naye akampuuza huyu, na mbora wao ni yule anaye anza kwa salamu".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- muislamu kumhama ndugu yake muislamu zaidi ya siku tatu, wanakutana wote hamsalimii wala hamsemeshi. Na mbora kati ya hawa wagomvi wawili ni yule anayejaribu kuondoa kuhamana huku, na akaanza kwa salamu, na makusudio ya kuhamana hapa ni sababu ya kujikweza, ama kuhamana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kama kuwahama waovu na wazushi na marafiki waovu, hili halina muda maalum, bali limeambatana na masilahi katika kuhama, na linamalizika kwa kuondoka maslilahi yake.

فوائد الحديث

Uhalali wa kumhama mtu ndani ya siku tatu kurudi chini, kwa kulinda maumbile ya kibinadamu, itasamehewa ndani ya siku tatu, ili kiondoke kile kilichojitokeza baina yao.

Ubora wa salamu, nakuwa huondoa yaliyoko ndani ya nafsi, nakuwa ni alama ya kupendana.

Pupa ya Uislamu juu ya udugu na ukaribu baina waislamu.

التصنيفات

Mambo mazuri na Adabu- Heshima., Kuhama na amasharti yake., Adabu za kuto asalamu na kubisha Hodi.