Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo

Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo

Kutoka kwa Samura bin Jundab na Mughira bin Shu'ba radhi za Allah ziwe juu yao, wamesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayesimulia kutoka kwangu mazungumzo ambayo yanaonekana kuwa ni uongo basi huyo ni mmoja kati ya waongo"

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayenukuu Hadithi kutoka kwake hali yakuwa anajua au anadhani au dhana yake kubwa kuwa ni kumzulia uongo rehema na amani ziwe juu yake; basi mpokezi atashirikiniana na mwanzilishi wa uongo huu katika dhambi.

فوائد الحديث

Kuzichunguza hadithi zinazopokelewa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kupata uhakika wa usahihi wake kabla ya kuzipokea na kuzisimulia.

Sifa ya uongo ataitwa kila aliyezusha uongo na kwa yule atakayeuhamisha na kuusambaza kwa watu wengine.

Ni haramu kusimulia Hadithi ya uzushi kwa mtu anayejua kuwa ni ya kutunga, au anayedhania kuwa ni ya kutunga, isipokuwa kama ni kwa ajili ya kutahadharisha.

التصنيفات

Umuhimu wa sunnah naNafasi yake., Tabia mbovu.