إعدادات العرض
Hakuna kujidhuru wala kusababisha madhara, na atakayedhuru Allah naye atamdhuru, na atakayemtia mtu uzito Mwenyezi Mungu atamtia uzito naye
Hakuna kujidhuru wala kusababisha madhara, na atakayedhuru Allah naye atamdhuru, na atakayemtia mtu uzito Mwenyezi Mungu atamtia uzito naye
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakuna kujidhuru wala kusababisha madhara, na atakayedhuru Allah naye atamdhuru, na atakayemtia mtu uzito Mwenyezi Mungu atamtia uzito naye".
[Ni sahihi kwa ushahidi wake] [Imepokelewa na Addaar- Alqutni]
الترجمة
العربية বাংলা Bosanski English Español Français Bahasa Indonesia Tagalog Türkçe اردو 中文 हिन्दी ئۇيغۇرچە Kurdî Hausa Português മലയാളം తెలుగు فارسی தமிழ் မြန်မာ Русский Deutsch 日本語 پښتو Tiếng Việt অসমীয়া Shqip Svenska Čeština ગુજરાતી አማርኛ Yorùbá Nederlands සිංහල ไทย دری Fulfulde Magyar Italiano ಕನ್ನಡ Кыргызча Lietuvių or Română Kinyarwanda Српски O‘zbek Moore नेपाली Malagasy тоҷикӣ Oromoo Wolof Soomaali Български Українська Azərbaycan ქართული bm Македонскиالشرح
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ni lazima kuzuia madhara kwa aina zake zote na sababu zake zote kwako na kwa wengine,ni haramu kwa yeyote kujiudhi mwenyewe na mwingine kwa kiwango sawa. Na ni haramu kwake kukabiliana na madhara kwa madhara; kwa sababu madhara hayaondoshwi kwa madhara, isipokuwa kama itakua katika njia ya kulipiza kisasi pasina kuvuka mipaka. Kisha akabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- adhabu pale yanapotokea madhara kwa mtu mwenye kuwadhuru watu, na pale zinapotokea tabu kwa mtu mwenye kuwatia watu tabu.فوائد الحديث
Katazo la kulipiza kwa zaidi ya vile ulivyofanyiwa.
Mwenyezi Mungu hakuwaamrisha waja wake lolote lenye kuwadhuru.
Katazo la kujidhuru au kudhuru ima kwa kauli au kitendo au kuacha.
Malipo hulingana na kitendo, atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakaye tia ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtia ugumu.
Katika kanuni za sheria: Ni "Madhara huondoshwa", Hivyo, sheria haikubaliani na madhara, na inakataza kujidhuru.
التصنيفات
Fomula za Kifq'hi na za Kiusulu.