Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu

Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu

kutoka kwa Abuu Swirma -Radhi za Allah ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayedhuru Mwenyezi Mungu naye atamdhuru, na atakayewatia watu ugumu Mwenyezi Mungu naye atamtilia ugumu".

[Ni nzuri] [Imepokelewa na Ibnu Maajah]

الشرح

Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutomuingizia madhara muislamu, au kumtia tabu katika jambo lolote katika mambo yake; Yeye mwenyewe au mali yake au familia yake, nakuwa atakayefanya hivyo basi Mwenyezi Mungu atamlipa na atamuadhibu kwa jinsi alivyomfanyia mwenzake.

فوائد الحديث

Uharamu wa kumdhuru muislamu na kumtia tabu.

Allah huwalipizia kisasi waja wake.

التصنيفات

Hukumu za Kupenda na Kuchukia., Hukumu za Kupenda na Kuchukia.