Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni

Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni

Imepokewa Kutoka kwa Abii Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu huyu muuaji anaeleweka, na vipi kuhusu muuliwaji? Akasema: "Hata yeye alikuwa na pupa ya kumuuwa mwenzake".

[Sahihi] [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

الشرح

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, akiwa na dhamira kila mmoja wao ya kummaliza mwenzake; Basi muuaji motoni kwa sababu ya kutekeleza mauaji ya kumuua mwenzake, Kuhusu muuliwaji, hilo likamtatiza Swahaba: Ni vipi anakuwa motoni? Akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hata yeye pia anakuwa motoni kwa sababu ya pupa yake ya kumuua mwenzake, na hakikumzuia kuuwa zaidi ya muuaji kumuwahi na kummaliza.

فوائد الحديث

Anastahiki adhabu mwenye kukusudia madhambi kwa moyo wake na akazifanya sababu zake.

Tahadhari kali ya kutopigana waislamu kwa waislamu, na kuna ahadi ya moto.

Mapigano kati ya waislam kwa haki hayaingii katika ahadi hii ya adhabu, mfano kama kuwapiga vita waasi na mafisadi.

Mwenye kutenda dhambi kubwa hakufuru kwa kulifanya pekee; Kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kawaita wenye kupigana kuwa ni waislamu.

Watakapokutana waislamu wawili kwa nyenzo yoyote miongoni mwa nyenzo za kuuwana, mmoja akamuunza mwenzake, basi muuwaji na muuliwaji wote motoni, na kutajwa panga katika hadithi ni sehemu ya mfano tu.

التصنيفات

Matendo ya moyoni., Kuyasema vibaya Maasi.