Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza

Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwatukane wafu, kwani wao tayari wameyapata yale waliyoyatanguliza".

[Sahihi] [Imepokelewa na Al-Bukhaariy]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- uharamu wa kuwatukana wafu na kuchafua heshima zao, nakuwa hili ni katika tabia mbaya, kwani wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza katika matendo mazuri au mabaya, kama ambavyo matusi haya hayawafikii basi hakuna lolote zaidi ya kuwaudhi waliohai.

فوائد الحديث

Hadithi ni ushahidi wa uharamu wa kuwatukana wafu.

Kuacha kuwatukana wafu kuna kuchunga masilahi ya waliohai, na kuhifadhi amani ya jamii kutokana na kutotiliana vinyongo na chuki.

Hekima ya kukatazwa kuwatukana nikuwa tayari wao wameyafikia yale waliyoyatanguliza, kuwatukana hakusaidii, na kuna kuwaudhi ndugu zake wa karibu.

Nikuwa haifai kwa mwanadamu kusema maneno yasiyo na manufaa.

التصنيفات

Mambo mazuri na Adabu- Heshima., Mauti na Hukumu zake.