Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni

Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni

Imepokewa kutoka kwa Farja -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema: "Yeyote atakaye kujieni hali yakuwa mmekubaliana kumfanya kiongozi mtu mmoja, akataka kupasua nguvu yenu, Au ausambaratishe umoja wenu, basi muuweni".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa waislamu watakapokubaliana juu ya kiongozi mmoja, na mshikamano mmoja, kisha akaja anayetaka kumpokonya madaraka, au akataka kuwasambaratisha waislamu kuwafanya kuwa makundi makundi, ni lazima wamzuie na wampige vita, kwa kuzuia shari yake, na kwa kuhifadhi damu za waislamu.

فوائد الحديث

Ulazima wa kumtii kiongozi anayesimamia mambo ya waislamu, katika mambo yasiyokuwa maasi, na uharamu wa kujitoa dhidi yake.

Atakayejitoa kwa kiongozi wa waislamu na umoja wao, basi ni wajibu kumpiga vita vyovyote vile itakavyokuwa nafasi yake ya cheo au ukoo.

Himizo la kuwa wamoja na kutofarakana na kuhitilafiana.

التصنيفات

Kutoka kwa ajili ya kumpinga kiongozi.