Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu

Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hakika Mwenyezi Mungu hatazami sura zenu na mali zenu, lakini anatazama katika nyoyo zenu na matendo yenu."

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hatazami sura za waja na miili yao, je ni nzuri au mbaya? Je ni mikubwa au midogo? Ina afya au maradhi? Na wala hatazami katika mali zao, je ni nyingi au kidogo? Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka hawaadhibu waja wake wala hawahesabu kwa mambo haya na kutofautiana kwao, lakini anatazama katika nyoyo zao na yale yaliyomo ndani miongoni mwa uchamungu na yakini, na ukweli na ikhlaswi, au ni lengo la kujionyesha au kutaka kusikika, na anatazama katika matendo yao upande wa usahihi wake au kuharibika kwake; Hapo atatoa thawabu na malipo kwa hayo.

فوائد الحديث

Kuwa na jukumu kubwa la kuirekebisha nafsi, na kuisafisha kutokana na kila sifa mbaya.

Moyo hutengemaa kwa Ikhlaswi, na matendo hutengemaa kwa kumfuata Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na sehemu hizi mbili ndio mahali pa kutazamwa na kuzingatiwa zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Mwanadamu asidanganyike kwa mali yake wala kwa uzuri wake wala kwa mwili wake wala kwa chochote miongoni mwa mionekano ya dunia.

Tahadhari ya kuridhika na mionekano, na kutorekebisha ndani ya moyo.

التصنيفات

Kumpwekesha Mwenyezi Mungu katika majina yake na sifa zake., Matendo ya moyoni.