Ewe Mola wangu! Yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawatia tabu, basi naye mtie tabu, na yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawahurumia, basi naye mhurumie

Ewe Mola wangu! Yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawatia tabu, basi naye mtie tabu, na yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawahurumia, basi naye mhurumie

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema ndani ya nyumba yangu hii: "Ewe Mola wangu! Yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawatia tabu, basi naye mtie tabu, na yeyote atakayesimamia lolote katika mambo ya umma wangu akawahurumia, basi naye mhurumie".

[Sahihi] [Imepokelewa na Imamu Muslim]

الشرح

Alimuombea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kila atakayesimamia jambo katika mambo ya waislamu liwe dogo au kubwa, sawa sawa usimamizi huu uwe ni wa umma, au sekta binafsi, na akawaingizia tabu na hakuwahurumia, kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amlipe kutokana na matendo yake, kwa kumtia matatizo na yeye. Nakuwa atakaye wahurumia na wakawafanyia wepesi, na akawarahisishia mambo yao basi Mwenyezi Mungu naye amuhurumie na ampe wepesi katika mambo yake.

فوائد الحديث

Ni wajibu kwa kila atakayesimamia lolote katika mambo ya waislamu awahurumie kiasi awezavyo.

Malipo huendana na matendo.

Mzani unaozingatiwa katika upole au ukali nikuwa usiende kinyume na Qur'ani na Sunna.

التصنيفات

Masharti ya kiongozi mkuu., Usamehevu wake Mtume Rehma na za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amani: