إعدادات العرض
1- Mwenye kuona miongoni mwenu jambo baya basi alibadilishe kwa mkono wake
2- Jihadi bora ni neno la uadilifu kwa kiongozi muovu
3- Mfano wa aliyesimama katika mipaka ya Mwenyezi Mungu na mwenye kuingia ndani yake, ni kama mfano wa watu waliotengeneza boti (safina) wakawa baadhi yao wako juu ya safina na wengine wako chini yake, na wakawa wale walioko chini yake wanapohitajia maji wanakwenda kwa wale walioko juu yao
4- Hakika watu watakapomuona mtu dhalimu (muovu) na wakawa hawakumzuia wako karibu mno, Mwenyezi Mungu kuwafunika wote kwa adhabu itokayo kwake
5- Namuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mtaamrisha mema, na mtakataza mabaya; au hakika atakuwa karibu zaidi Mwenyezi Mungu kukutumieni adhabu toka kwake, kisha mtamuomba na wala hamtojibiwa