إعدادات العرض
1- Shikamaneni na hii Qur'ani, Namuapa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mkononi mwake, hiyo ni nyepesi sana kuponyoka kuliko ngamia kuponyoka kutoka kwenye kamba yake.
2- Mbora wenu ni yule aliyejifunza Qur'ani na akaifundisha
3- Msizifanye nyumba zenu kuwa makaburi, hakika shetani huikimbia nyumba
4- Atakayezisoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara katika wakati wa usiku zitamtosheleza
5- Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja na jema hilo kwa mema kumi mfano wake
6- Alikuwa Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akimtaja Mwenyezi Mungu katika nyakati zake zote.
7- Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Nimeigawa swala baina yangu na mja wangu nusu mbili, na mja wangu ana haki ya kupata alichooomba
8- Kilipomfikia Abuu Twalib kifo, Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- alimuendea akamkuta Abdullahi bin Abii Umaiyya na Abuu Jahli wakiwa wake, Akasema kumwambia mgonjwa: Ewe baba mdogo, Sema Laa ilaaha illa llaah -Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu-, neno ambalo nitakutetea kwalo kwa Mwenyezi Mungu.
9- Mfano wa muumini mwenye kusoma Qur'ani ni kama mfano wa chenza harufu yake nzuri na ladha yake nzuri, na mfano wa muumini ambaye hasomi Qur'ani ni kama mfano wa tende: haina harufu na ladha yake ni tamu
10- Hakita simama Kiyama mpaka jua lichomoze kutoka upande wa Magharibi, na likichomoza na wakaliona watu wote wataamini
11- Mauti yataletwa yakiwa kama dume la Kondoo mwenye rangi mchanganyiko ya weusi na weupe
12- Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli wala ni waongo, na semeni hivi {Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yote yaliyoteremshwa kwetu sisi}
13- Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hajui kitenganishi kati ya Sura na Sura nyingine mpaka imteremkie {Bismillahir Rahmanir Rahiim}
14- Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma
15- walikuwa wakitusomea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hivyo hawakuwa wakichukua Aya kumi zingine mpaka wawe wamekwishayafanyia kazi yaliyo ndani ya aya hizo kumi kwa kujifunza na kuyafanyia kazi
16- Ewe baba Mundhir, hivi unaijua aya gani katika kitabu cha Mwenyezi Mungu ambayo ni tukufu zaidi?" Akasema: Nikasema: {Allahu laa ilaaha illa huwal hayyul qayyuum} Al-baqara: Basi akanipiga katika kifua changu, akasema: Nakuombea Mwenyezi Mungu elimu ikupe furaha ewe baba Mundhir
17- Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapolala kitandani kwake wakati wa kila usiku alikuwa akikusanya viganja vyake, kisha akivipuliza na kuvisomea : {Qul-huwallahu Ahad}, na {Qul-A uudhu birabbil falaq} na (Qul-Auudhu birabbi naas }
18- Mayahudi wameghadhibikiwa, na Wakristo ni wapotofu
19- Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya
20- Akasema: "Watahesabiwa kwa hiyana waliyokufanyia na kukuasi na kukudanganya, na itahesabiwa adhabu yako uliyowapa
21- Hakika haya unayoyasema na kuwalingania watu ni mambo mazuri, ikiwa utatwambia juu ya haya tuliyoyafanya kama yana kafara
22- Enyi watu hakika Mwenyezi Mungu ameondosha kwenu nyinyi kiburi cha zama za ujinga, na kujifaharisha kwa nasaba
23- Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema