إعدادات العرض
1- Dinari moja unayoitoa kwenye njia ya Allah, na dinari moja unayoitoa kwa mtumwa, na dinari moja unayoitoa sadaka kwa masikini, na dinari moja unayoitoa kwa familia yako, yenye malipo makubwa kuliko yote ni ile unayoitoa kwa familia yako
2- Hana swaumu atakayefunga milele, na funga ya siku tatu ni sawa na kufunga mwaka mzima
3- Atakayeandaa mnyama kwa ajili ya kuchinja, na ukaandama mwandamo wa mwezi Dhul Hija, basi asipunguze chochote katika nywele zake wala kucha zake mpaka atakapochinja mnyama wake wa Udh-hiya
4- Inapokuja Ramadhani hufunguliwa milango ya pepo na hufungwa milango ya moto, na mashetani hufungwa minyororo
5- Lau wangejua watu waliyomo katika Adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate nafasi ila kwa kupiga kura ili kuyafikia basi wangelipiga kura
6- Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake
7- (Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume